Mke wa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, Edward Lowassa, Regina Lowassa amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2020 yanapaswa kuanza mapema.

Hayo ameyazungumza jana mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake wa Chadema (Bawacha) mjini Dodoma.

Mama Regima Lowassa amewataka wajumbe kujiamini zaidi na kupeleka ujumbe kwa wenzao ambao wamedhamiria kufanya mageuzi makubwa lakini akawataka wasilale.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee aliwataka wanawake kujitoa zaidi katika kukisaidia chama hicho, hasa katika maandalizi ya uchaguzi ujao.

Mdee aliwashauri wanawake wenye nafasi, kama wabunge, kutumia nafasi zao kukisaidia chama.

Alisema wakati walionao kwa sasa si wa kujivunia nafasi walizonazo, bali wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na kugombea nafasi za uongozi wa juu wa Chadema ili waendeleze mapambano ya ukombozi.

Katika kuonyesha msisitizo huo, alimuagiza katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega kuwaandikia barua wabunge ambao hawakuhudhuria kikao cha jana ili wajieleze kabla ya kuchukuliwa hatua.

Alisema ni jambo la aibu na fedheha kwa viongozi kutoka mbali wakasafiri hadi Dodoma kwa ajili ya kikao, lakini wabunge ambao wako mjini hapa wakashindwa kuhudhuria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *