Mke wa muuza madawa maarufu nchini Mexico, Joaquin Guzman ‘El Chapo’ anayeitwa Emma Coronel Aispuro amezuiliwa kumtembelea na kumuona mumewe ambaye yupo gerezani nchini Marekani.

Mawakili wake wanasema kuwa mkewe amezuiliwa kumtembelea tangu asafirishwe chini ya ulinzi mkali kutoka Mexico mwezi uliopita.

Guzman, ambaye amefanikiwa kutoroka mara mbili kutoka magereza ya Mexico, aliwahi kutoroka kupitia kikapu kikubwa na mara ya pili alichimba shimo kubwa chini ya ardhi kupitia seli yake.

Hivi sasa anazuiliwa akiwa pekee katika gereza lenye ulinzi mkali jijini New Yor huku muda mwingi Guzman haruhusiwi kukaaa na wafungwa wengine kuhofia usalama wake.

Guzman anashtakiwa kwa kuwa na silaha kinyume cha sheria ya ulagunzi wa madawa ya kulevya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *