Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaachia watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya dada wa Bilionea Erasto Msuya jana baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kugoma kuifanyia mabadiliko hati ya mashtaka, mahakama hiyo imewapandisha tena kizimbani na kusomewa mashtaka yale yale.

Mbele ya Hakimu Thomas Simba, upande wa jamhuri ukiongozwa na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Helen Mushi ambapo Wakili kishenyi alidai watuhumiwa Miriam Msuya na Revocatus Muyela kuwa Mei 25, mwaka jana huko eneo la Kigamboni Kibada, jijini Dar es Salaam ambapo walimuua kwa kumchinja dada wa bilionea huyo, Anet Msuya

Hakimu Simba alisema mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo hadi upelelezi utakapokamilika ihamishiwe Mahakama Kuu.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala uliomba mahakama hiyo kuwasilisha hoja za wateja wake kuachiwa kama uamuzi wa mahakama ulivyofanya jana kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kutekeleza amri ya mahakama iliyowataka kurekebisha hati ya mashtaka.

Upande wa mashtaka ulidai sababu zilizotolewa na Kibatala hazina ushahidi kwa sababu hajarejea kifungu maalumu cha kutaka watuhumiwa kuachiwa huru. Baada ya kuwasiliaha hoja za upande zote mbili mahakama imesema itapitia hoja hizo kisha Machi 7, mwaka huu itatoa uamuzi hivyo watuhumiwa walirudishwa mahabusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *