Staa wa  muziki kutoka nchini Nigeria, Omo Jagabana ‘YCEE’ ametoa msaada wa shilingi milioni moja kwenye kituo cha kulelea watoto waishio mazingira magumu cha Kigamboni Community Center (KCC).

Mratibu wa ujio wa msanii huyo Salha Kibwana amesema kwamba YCEE ametoa msaaada huyo katika kituo hiko kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji maalumu ya kila siku katika kituo hiko.

Pia Salha amesema msanii huyo ametoa msaada huo kutokana na faida anayopata kwenye kazi yake ya muziki ili kukuza vipaji na upatikanaji wa elimu katika jamii hasa watoto waishio katika mazingira magumu.

kwa upande wake mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule amesema anashukuru sana msaada kutoka kwa msanii huyo kutokana na kituo chake kulea watoto wengi na wanahitaji msaada.

Pia msanii huyo amesema kwamba amekuja Tanzania kujifunza na kuja kuonana na wasanii pamoja na kusaidai jamii zenye mazingira magumu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *