Mjumbe wa Baraza la Congress nchini Marekani, Steve King-R amewatembelea wanafunzi wa Lucky Vicent wanaopata matibabu nchini humo.
Kiongozi huo amefika hospitali ya Mercy walipolazwa wanafunzi hao kwa ajili ya kuwajulia hali baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na ajali ya gari walioipata wilayani Karatu mkoani Arusha mwanzoni mwa mwezi huu.
Mjumbe huyo alipata furasa ya kuzungumza na wanafunzi hao ambao kwasasa hali zao zimeanza kuimarika kutokana na huduma wanazopata kwenye hospitali hiyo ya Mercy nchini Marekani baada ya kusafirishwa wiki kadhaa zilizopita.
Wanafunzi hao walinusurika kwenye ajali iliyoua wanafunzi wenzao 32 walimu wawili na dereva wa gari hilo.
Ajali hiyo imetokea Mei 6 mwaka huu ambapo wanafunzi walikuwa wanaenda Karatu kwa ajili ya kufanya mitihani ya ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa shule ya misingi Tumaini iliyopo wilayani Karatu.