Mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi, marehemu Kepteni John Komba, Salome Komba amemwomba Rais Magufuli kumsaidia  ili aweze kulipwa mirathi ya mume wake Sh milioni 75.

Komba ambaye alikuwa Muhamasishaji na Mkurugenzi wa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), inayomilikiwa na CCM alifariki dunia mwaka juzi katika Hospitali ya TMJ baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Mjane huyo amesema kuwa fedha hizo ni mirathi inayotokana na bendi ya TOT ambayo mumewe alikua mkurugenzi wake tangu alipokuwa kada wa chama hicho hadi alipofariki mwaka 2015.

Amesema mara baada ya mumewe kufariki, aliweza kufuatilia mirathi hiyo ambayo mpaka sasa amelipwa Sh milioni 4.5 badala ya Sh milioni 75,  ambapo hadi sasa familia bado inadai kiasi hicho cha fedha.

Pia amesema kutokana na hali hiyo, aliweza kuzungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kumweleza kama anadai fedha hizo na amelipwa Sh milioni 4.5 tu.

Ameongza kwa kusema kuwa marehemu kabla ya kufariki alikuwa anaipenda CCM na kabla alidiriki kuhamasisha wasanii wenzake kuhusiana na kampeni.

Mwisho amemalizia kwa kusema kutokana na hali hiyo, alimwomba Rais kumsaidia suala hilo kwa sababu ni jasho la mumewe  na ni haki yake kwa kazi alizozifanya wakati wa uhai wake na kwa jinsi alivyoweza kujitoa ndani ya chama hicho na kwamba mpaka anafariki alikuwa mwana CCM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *