Shindano la Miss Tanzania ambalo lilikuwa limesimama kwa muda kidogo limerejea kwa kasi ya aina yake ambapo mwaka huu shindano hilo litafanyika jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari Kamati ya Miss Tanzania mwaka 2016 Hidan Ricco wakati wa ziara ya mafunzo kwa warembo hao.

Washiriki hao tayari wameingia kambini kwa ajili ya kuanza safari ya kulisaka taji lla Miss Tanzania 2016 katika shindano hilo lenye msisimko wa aina yake.

Kwa mujibu wa Ricco washiriki wa shindano hilo ambao wamepatikana kwa mchujo uliofanyika mikoani watakuwa na semina na ziara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja Dodoma, Singida, Geita na Mwanza ili kuweza kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Tanzania.

Shindano hilo tayari limeanza kwa washiriki kuwa kambini kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 29 fainali itakapofanyika Jijini Mwanza na mshindi kutangazwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *