Miss Tanzania 2016, Diana Edward amewashangaa baadhi ya watu kuponda gari alilopewa kuwa lina mapango mengi ya matangazo.
Kauli ya miss huyo imekuja baada ya watu kwenye mitandao ya kijamii kukejeli gari hilo na kusema kuwa lina matangazo mengi kwa hiyo linamuonekana mbaya na limepoteza mvuto.
Diana amesema kuwa mabango hayo yatatolewa siku mbili zijazo kwa hiyo hayana tatizo kuwepo kwenye gari hilo kwasasa tofauti na watu wanavyoponda zawadi hiyo kwenye mitandao ya kijamii.
Mrembo huyo amesema kuwa anatoa shukrani na anawaunga mkono waandaaji na hawezi kuwazuia watu kusema kwa kuwa hawafahamu namna gani wamepambana kulipata gari hilo.
Diana amesema kuwa anawaunga mkono waandaaji wa shindano hilo kwa kumpatia gari lake na hawezi kuwasema vibaya kutokana wamepambana mpaka kulipata gari hilo.
Mrembo huyo amemalizaWatu hawawezi kujua kwa sababu wapo kwenye social media, lakini wangekuwepo tangu watu wanahangaika kulipata hilo gari tangu mwezi wa 6 mpaka leo hii wmaepata.