Shindano ya Miss World mwaka huu yamefikia tamati huku Miss Puerto Rico, Stephanie Del Valle ameibuka na ushindi kwenye shindano hilo baada ya kuwashinda marembo wenzake walioshiriki.

Shindano hilo limeshirikisha warembo 116 kutoka nchi mbali mbali duniani ambapo limefanyika katika jiji la Washington DC nchini Marekani na kuhudhuriwa na wapenzi wa urembo duniani kote.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Yarutza Miguelina Reyes Ramirez kutoka nchi ya Dominican huku nafasi ya tatu ikienda kwa Natasha Mannuela kutoka nchini Indonesia ambao walifanikiwa kuingia nafasi tatu za juu.

Kwa upande wa nchi ya Afrika Kenya imefanikiwa kuingia tano bora kwenye mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.

Ikumbukwe kuwa Tanzania iliwakilishwa na mrembo Diana Edward ambaye hakufanya vizuri kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kuingia hata nafasi ya 20 bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *