Timu ya taifa ya Misri imefanikiwa kutinga fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuifunga Burkina Faso kwa jumla ya penati 4-3.

Katika dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na kupelekea kuongezwa kwa dakika za zaida kabla ya kupigwa kwa penati.

Misri ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli baada ya mshambuliaji wake Mohammed Salah kupiga shuti na kumshinda mlanda mlango Herve Koffi na mpira huo kuingia nyavuni katika dakika 66.

Goli la kusawazisha la Burkina Faso lilifungwa na mshambuliaji wake Bance katika dakika 73 ya mchezo huo.

Shuja wa Misri kwa mechi ya jana alikuwa mlinda mlango wao mkongwe, Essam El Hadary ambapo amefanikiwa kuokoa mikwaju miwili ya penati.

Nusu Fainali nyingine itafanyika leo kati ya timu ya Ghana itakapopambana na Cameroon kwenye nusu fainali ya pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *