Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema Tanzania imekubaliana na serikali ya Misri kuja kuanzisha kiwanda kikubwa cha nyama ili kukuza ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.

Tanzania na Misri zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya Kiuchumi, Elimu, Afya na Utalii.

Makubaliano hayo ni miongoni mwa mikataba kadhaa iliyotiwa saini kati ya Rais Magufuli na mgeni wake Rais Abdel Fattah – al Sisi wa Misri aliyewasili nchini leo mchana kwa ziara ya siku mbili.

Ziara ya Rais al – Sisi ina lengo la kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Misri na pia kutoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadili masuala mbalimbali yanaohusu nchi hizo mbili ya kikanda na kimataifa.

Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini, Tic, kimesajili jumla ya miradi nane kutoka Misri kati ya mwaka 1990 hadi 2017, miradi hiyo ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani milioni 887.02 na kutoa ajira zipatazo 953, uwekezaji huo ukiwa katika maeneo ya Kilimo, viwanda vya mbao, mbolea, madini, na sekta ya Huduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *