Msanii wa muziki ambaye yupo chini la ya kampuni ya filamu ya Wema Sepetu ‘Endless Film’, Mirror, amesema kukaa ndani ya kampuni hiyo kwa muda mrefu kumemfanya atamani kuigiza.

Wema-na-Mirror

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Mirror amesema ipo siku mashabiki wake watashangaa ameibukia kwenye uwigizaji.

“Nimekaa kwa muda mrefu sana Endless Film, chini ya Wema, na yeye ni mwigizaji mzuri sana, kwa hiyo katika hali ya kawaida lazima uvutiwe tu,” alisema Mirror.

“Kama mimi sasa hivi napenda kuigiza, natamani hata nipate nafasi ya kuonyesha uwezo wangu,” aliongeza Mirror.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo wa wimbo ‘Baby’ amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya project yake mpya na Ommy Dimpoz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *