Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amefunguka na kuwachana baadhi ya mashabiki wa Bongo Fleva waliombeza baada ya baada ya kupunguza mwili wake.

Baadhi ya mashabiki wake hawakupendezwa na jambo hilo ila kwa upande wake wanapaswa kusikiliza muziki wake na sio kujikita zaidi katika muonekano wake.

Mimi Mars amesema kuwa alilazimika kufanya hivyo ili kujiongezea kujiamini zaidi katika tasnia ya muziki na pia muonekano wa awali alikuwa hapendezwi nao.

Amesema kuwa hajafurahi na nilichokuwa nakiona ilikuwa inamnyima confidence kidogo kutokana na mashabiki hao.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Papara’ ameongeza kuwa alitumia muda wa miezi minne hadi mitano kupata muonekano alionao kwa sasa kwa kubadilisha mfumo wa kula na kufanya mazoezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *