Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marianne Mdee (Mimi Mars) amesema kuwa waigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu na Elizabeth Michael ‘Lulu’ walikataa kumshirikisha kwenye movie yao.

Mimi Mars ambaye ni mdogo wake na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ameendelea kusema kuwa licha ya changamoto hiyo aliyokutana nao lakini hakukata tamaa katika maisha yeke.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa licha ya hayo yote kutokea lakini hana toafuti na waigizaji hao kwasasa ni marafiki zake ambao wanasaidia katika mambo mengi.

 Pia ameongeza kwa kusema kuwa amepitia vikwazo vingi katika kutafuta mafanikio kama ambavyo wasanii wengine wamepitia licha ya yeye kuwa mdogo wake na Vanessa Mdee.

“Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini, Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga chini fulani hivi but it’s okay,”
.

Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha TV One kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Shuga’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na TV nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *