Waziri wa Nchi Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama ameiagiza Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kutoa taarifa haraka kuhusu malipo hewa ya wastaafu.

Mhagama amesema taarifa za malipo hewa ya mafao yakustaafu zinahitajika haraka ili ziambatanishwe na ripoti ya watumishi hewa na zifanyiwe maamuzi ili kuokoa pesa ambazo wangelipwa watumishi hewa na kulisababishia taifa hasara ya fedha ambazo kama zitapelekwa kwenye huduma za jamii zingepunguza umasikini.

Pia amesema kuwa serikali imeagiza mashirika yote ya hifadhi ya jamii yaanze kutekeleza miradi yenye tija kwa watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa nafasi za ajira na kuwaajiri watanzania wenye sifa na kuwaongezea kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Waziri huyo amesema kwamba taarifa hiyo inatakiwa haraka ili iambatanishwe na ripoti ya wafanyakazi hewa itakayowezesha kuwatambua watumishi halali na kuwapatia stahiki zao huku wale watakaobainika kufanya udanganyifu wachukuliwe hatua za kisheria.

Hiyo ni tofauti na sasa ambapo mashirika hayo yamewekeza zaidi kwenye majengo ya kupangisha kwa gharama kubwa na kusababisha wananchi wa vipato cha chini kulalamika kwa kutoona faida za mifuko hiyo ya jamii ambapo kila mwezi hukatwa fedha zao kwaajili ya mifuko hiyo ya jamii.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *