Hatimaye madada ndugu, Venus na Serena Williams wanakutana tena kwenye fainali kubwa kwa mara ya tisa kwenye historia yao ya kucheza Tennis.

Hadi kufika hapo, dada mkubwa Venus mwenye miaka 36, alimshinda Mmarekani mwenzake Coco Vandeweghe kwa seti 6-7 (3-7) 6-2 6-3 nakufika fainali yake kubwa ya kwanza tangu mwaka 2009.

Serena anayeshika nafasi ya pili kwa ubora wa viwango duniani, huku akiwa na umri wa miaka 35, alimshinda mpinzani wake ambaye hana jina kubwa Mirjana Lucic-Baroni raia wa Croatia kwa seti 6-2 6-1.

Endapo Serena atamshinda dadaake kwenye fainali hiyo, ataandika historia ya kushinda mara 23 Grand Slam kwa wachezaji mmoja mmoja.

Wakati huo huo ushindi kwa Venus utakuwa ni ubingwa wa nane wa mashindano makubwa tangu aliposhinda ubingwa mkubwa mwaka 2008 kwenye mashindano ya Wimbledon.

‘Ni kitu kinachofurahisha sana kumtazama Serena namna anavyocheza Tennis, namna anavyopiga mpira na namna alivyomshindani. Itakuwa pambano gumu kati yetu’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *