Aliyekuwa star wa NBA, Michael Jordan ameshinda kesi dhidi ya kampuni ya China iliyokuwa inatumia jina lake kujiingizia kipato.

Mahakama kuu ya nchini China imempa ushindi Jordan katika Kesi hiyo baada ya kuonekana kampuni hiyo ilifanya makosa ya kutumia jina lake bila ruhusa yake.

Michael Jordan tangu mwaka 2012 alianza malalamiko dhidi ya Kampuni ya Qiaodan Sports.

Ampapo kampuni hiyo ilikuwa ikitumia jina lake kuuza bidhaa zenye jina la Jordan lakini kwa kichina Chee-ow-dahn.

Mchezaji huyu amesema amefurahi kuona jina lake linaheshimiwa.

Mahakama hiyo imewaambia wachina wasitumie hilo jina la Jordan kwa kichina lakini wamewaachia mwanya kuwa wanaweza kuandika jina hilo kwa herufi za kirumi Qiaodan Chee-ow-dahn.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *