Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Michael Ballack amemshauri kiungo wa Arsenal Mesut Ozil kuihama klabu hiyo endapo anahitaji mafanikio ya kutwaa mataji mbali mbali.

Ballack mwenye umri wa miaka 40 ambaye aliwahi kukipiga na Chelsea ya Uingereza amesema Ozil amekua na wakati mgumu wa kuutendea haki uwezo wake wa kucheza soka tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Katika ushauri huo Ballack amemtaka kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani kujiunga na klabu ya Bayern Munich ambayo ni klabu iliyozoea kubeba makombe tofauti na Arsenal.

arsenal-fc

Mkataba wa Arsenal na mchezaji huyo umebakia miezi 18 kufikia mwisho na kuna uwezokano wa Ozil kutosaini mktaba mpya na The Gurnes.

Timu alizowahi kucheza Ozil kabla ya kujiunga na Arsenal ni Schalke 04 na Werder Bremen kabla ya kutimkia Hispania kujiunga na Real Madrid, ambapo alitwaa ubingwa wa ligi (La Liga) na kombe la Mfalme (Copa del Rey).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *