Leo September 13 ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa mwanamuziki nyota wa hip hop nchini Marekani, Tupac Amaru Shakur  ‘2Pac’ ambapo alifariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Mwanamuziki huyo alipigwa risasi na watu wasiojulikana mnamo tarehe kama ya leo mwaka 1996 katika jiji la Las Vegas nchini Marekani na kupelekea kufariki dunia wakati akiwaishwa hospitali.

2pac alijizolea umaarufu mkubwa duniani kote kupitia kazi zake za muziki baada ya vibao vyake kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani na nje ya Marekani.

2pac pia alikuwa anafanya kazi na mtayarishaji wa muziki maarufu nchini Marekani Dr. Dre ambapo ndiyo aliyekuwa anaandaa nyimbo zote za mwanamuziki huyo enzi za uhai wake.

Baadhi ya nyimbo za 2pac zilizobamba wakati wa uhai wake ni Dear Mama, California Love, Life Goes On, Hit Em Up pamoja na Hail Maily ambazo zilikuwa moto wa kuotea mbali wakati huo.

Pia Albamu alizowahi kutoa 2pac ni All Eyez On Me, The Don Killuminati pamoja na The 7 day Theory zilizofanikiwa kusambaa dunia nzima.

Kifo cha 2pac kinahusishwa na ugomvi uliokuwepo kati ya kundi lake na kundi la aliyekuwa rapa mwenzake BIG Notorius ambaye pia ni marehemu kutokana na kutokuwa na maelewano baina ya watu hao wawili.

2pac na BIG Notorius ni miongoni mwa wana hip hop walioleta mapinduzi makubwa sana enzi za uhai wao kutokana na kufanya harakati za kutetea watu weusi wa Marekani pamoja na ngoma zao kubamba nyoyo za mashabiki wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *