Hakimu Deen Potter wa nchini Australia amemtaka kijana mmoja kumuiga mwanamuziki wa Marekani, 50 Cent ili kuepuka maisha ya uhalifu.

Hakimu huyo ametoa ushauri huo kwa kijana huyo wakati alipokuwa akimhukumu kwenda jela kutokana na kosa la wizi.

Hakimu huyo alimtaka kijana huyo kumuiga 50 Cent kwasababu mwanamuziki huyo alikuwa anaishi maisha ya uhalifu na kuuza dawa za kulevya kabla ajawa staa wa muziki lakini kwasasa ameacha tabia hiyo na anaendelea na maisha ya kawaida.

Hakimu huyo aliendelea kumwambia kijana huyo “Katika kipindi cha miaka 10 ijayo nataka kukuangalia na kuona mafanikio yako”.

Kijana huyo alikuwa anakabiliwa na mashataka 49 baada ya kuiba mali yenye zaidi ya thamnai ya dola 7,000 nchini Australia.

Hakimu huyo amesema ”Katika kipindi cha miaka 10 ijayo nataka kukuangalia na kuona mafanikio yako”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *