Mshambuliaji wa Simba SC, Mussa Hassan “Mgosi” amestaafu rasmi soka na sasa anakuwa Meneja wa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa Taifa dhidi ya URA kutoka Uganda.

Manara ameeleza kwamba aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Ally anakuwa Mratibu wa timu  kuanzia leo na nahodha mpya ni Jonas Mkude.

Kiungo wa klabu hiyo, .

Simba watacheza dhdi ya URA ili kuwapa nafasi mashabiki wao kukiona kikosi chao kwa mara ya pili baada ya kikosi hicho kutakataka kwenye maadhimisho ya siku ya Simba maarufu kama SIMBA DAY ambapo waliichapa timu ya AFC Leopard ya Kenya kwa mabao 4-0 .

Wakati huo huo, Wekundu wa Msimbazi, Simba wamemtoa kwa mkopo kiungo wao Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC.

Mwalyanzi amejiunga na timu iliyopanda daraja msimu huu ya African Lyon.

Samba inatarajia kufuangua ligi Agosti 20 kwa mechi dhidi ya Ndanda FC kwenye mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *