Mgonjwa Neema Wambura ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) amemshukuru Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake kuimarika na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Neema amemshukuru rais kwa kumwezesha kupata matibabu tangu alipofikishwa katika hospitali hiyo Februari 23, mwaka huu.

Pia, Neema amewashukuru madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwa kumpatia huduma bora na kumwezesha kupona majeraha ya moto.

Neema ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Mara alimwagiwa maji ya moto na mumewe wakati alipokuwa akichemsha maji kwa ajili ya kupika ugali na kuungua sehemu ya kifuani, shingo na mkono.

Mkuu wa Idara ya Upasuaji na Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dk Ibrahim Mkoma  amesema afya ya Neema inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji sehemu ya shingoni ili kutenganisha shingo na sehemu ya kifua na kuziba majera ya moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *