Kampuni ya Acacia imesema kuwa mmoja wa wafanyakazi wake wa kimataifa anayefanya kazi naΒ Pangea Minerals Limited amezuiwa kuondoka Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Acacia wameeleza kuwa, mfanyakazi huyo ambaye hawakumtaja jina alikamatwa na hati yake ya kusafiria ilichukuliwa huku na yeye akishikiliwa kwa muda.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya kampuni hiyo, Acacia wamedai kuwa baada ya kuingilia sakata hilo kisheria, mfanyakazi huyo aliachiwa na hati yake ya kusafiria ikarejeshwa.
Aidha, wamesema tukio hilo limetokea kipindi ambacho kwa takribani siku mbili sasa wafanyakazi wake wamekuwa wakisumbuliwa na maafisa mbalimbali wa serikali.
Kuhusu tuhuma hizo, serikali kupitia kuwa Msemaji Mkuu, Hassab Abas imesema kuwa inafuatilia tuhuma hizo na baada ya muda mfupi watatoa taarifa kamili.