Mfanyabiashara wa pombe za viroba mkoani Dodoma, Festo Mselia amejiua baada ya Jeshi la Polisi mkoani humo kukamata shehena ya pombe kali za viroba kwenye ghala la Kampuni yake Mselia Enterprises.

Mfanyabaishara huyo ni wakala mkuu wa usambazaji wa pombe hizo ambapo alikuwa akimiliki shehena ya pombe hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1, kukiwa na zaidi ya katoni 1400 za viroba katika moja ya stoo zake.

Awali katika operesheni hiyo iliongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa ambapo alimtaka aendelee na shughuli zake na akaamuru shehena hiyo isiuzwe wala kutumika akisubiri maelekezo.

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limedai kuwa taarifa rasmi juu ya tukio la mfanyabiashara huyo itatolewa mara baada ya uchunguzi rasmi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *