Mfalme Mohammed VI wa Morocco anatarajiwa kuwasili leo nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya Morocco na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga, amesema baada ya ziara rasmi mfalme huyo atakuwa na likizo na atatembelea sehemu mbalimbali ikiwa ni matembezi binafsi.

Pia, atatembelea Zanzibar na kukutana na Rais Ali Mohamed Shein na pia atatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Mfalme huyo pia atatembelea taasisi za kidini, ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti wa Kinondoni, na kukutana na viongozi wa dini ya Kiislamu na ataswali sala ya Ijumaa huko Zanzibar.

Mfalme Mohammed VI na Rais John Pombe Magufuli wanatarajiwa kusaini makubaliano 11 ya ushirikiano katika sekta za kilimo, gesi, mafuta, reli ya Liganga na Mchuchuma na sekta ya utalii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *