Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morroco, Mohammed VI wamesaini mikataba 21 ya ushirikiano wa maendeleo.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa amemuomba mfalme huyo kujenga uwanja huo ambao utakuwa mkubwa zaidi ya Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema “Nimemuomba Mfalme ajenge msikiti mkubwa hapa jijini Dar es Salaam. Lakini pia nimemuomba atujengee uwanja mkubwa wa mpira Dodoma ambao utagharimu kiasi cha dola milioni 100 ambao utakuwa mkubwa zaidi ya huu wa taifa, vyote amekubali atajenga,”.

Uwanja huo utatarajiwa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu sitini ambao ndiyo idadi ya mashabiki inayochukuwa kwa sasa uwanja wa taifa wa jijini Dar es Salaam. Mfalme huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *