Mfalme wa Morocco, Mohammed VI amewasili nchini akiwa na msafara wa ndege tano zilizobeba vifaa vyake ikiwemo vitanda na mazulia ya kifalme.

Mfalme huyo aliwasili jana saa 11:15 jioni akiwa na ujumbe wake wa watu zaidi ya 150 wakitokea nchini Rwanda.

Kabla ya kuwasili kwa ndege yake zilitangulia ndege mbili ndogo za Morocco zilizokuwa na ujmbe ulioambatana naye.

Mfalime Mohammed alipokelewa uwanja wa ndege na vikundi mbali mbali vya ngoma pamoja na raia wa Morocco wanaoishi hapa nchini.

Ulinzi uliimarishwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport kwa maofisa wa pande zote mbili waliozunguka uwanjani hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *