Mfalme wa Morocco, Mohammed VI wa Morocco jana amewasili visiwani Zanzibar ambako akitokea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara katika ardhi ya Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mfalme Mohammed VI aliagwa na mwenyeji wake, Rais John Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Akiwa jijini Dar es Salaam, Mfalme Mohammed VI aliyewasili nchini Oktoba 23, mwaka huu kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli na pia viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mfalme Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *