Terry Gobanga, wakati huo akiitwa Terry Apudo alipotoweka katika harusi yake hakuna mtu aliyedhani kwamba alitekwa nyara ,kubakwa na kutuwa kandakando ya barabara akipigania uhai.

Lilikuwa janga la kwanza kati ya mawili kumkabili muhubiri huyo kijana .Lakini ni manusura.

Harusi iliopangwa ilitarajiwa kuwa harusi kubwa.

Nilikuwa muhubiri hivyobasi wanachama wote wa kanisa walitarajiwa kuhudhuria.

Mchumba wangu ,Harry na mimi tulikuwa na furaha tulikuwa tunafunga ndoa katika kanisa la All Saints Cathedral mjini Nairobi na nilikuwa nimekodisha rinda zuri sana la harusi.

Lakini usiku kabla ya ndoa yetu ,niligundua kwamba nina baadhi ya nguo za Harry .

Hakuweza kuja katika harusi bila tai kwa hivyo rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa amekubali kubaki nami usiku wa kuamkia harusi alikubali kumpelekea mapema alfajiri.

Haki miliki ya picha Terry Gobanga Image caption Terry Gobanga

Niliamka mapema na kumpeleka hadi katika kituo cha kupanda basi.

Nilipokuwa nikirudi nyumbani ,nilipita karibu na mtu mmoja ambaye alikuwa ameketi kati boneti ya gari na akanishika kutoka nyuma na kuniingiza katika viti vya nyuma vya gari hilo na kuondoka mahali hapo.

Yote haya yalifanyika katika chini ya sekunde moja .Nilifunguliwa mdomo na kuwekwa kipande cha nguo mdomoni.

Nilikuwa nikirusha mikono na miguu nikitaka kupiga kelele.Nilipofanikiwa kutoa kitambara hicho nilipiga kelele: Ni siku yangu ya harusi! hapo ndipo nilipopigwa ngumi .

Mmoja ya wanaume hao wakaniambia nishirikiane nao ama niuwawe.Wanaume hao walinibaka kwa zamu .

Nilihisi nitafariki ,lakini bado niliendelea kupigania uhai wangu, hivyobasi mtu mmoja alipotoa kitambara kilichokuwa mdomoni mwangu nilimuuma uume wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *