Mshindi wa wa pili wa shindano la kutafuta vipaji ‘ American’s Got Telent 2010’, Jackie Evancho anatarajia kuongoza wimbo wa taifa wakati wa kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump mwezi Januari.

Msichana huyo wa miaka 16 amesema ana furaha sana kwamba atakuwa anaongoza wimbo huo wa taifa wakati wa sherehe hiyo tarehe 20 Januari.

Boris Epshteyn, mkurugenzi wa mawasiliano wa kamati inayofanya maandalizi ya sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Bw Trump amesema msichana huyo anawapa moyo Wamarekani wote.

Mwanamuziki wa Italia, Andrea Bocelli na Kanye West ni miongoni mwa wasanii wengine ambao inadaiwa huenda wakatumbuiza siku hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *