Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amechukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene inasema kuwa kiongozi huyo ambaye alikuwa ameambatana na viongozi wengine wa Chama madiwani wa CHADEMA wamezuiliwa na jeshi la polisi maeneo ya Halmshauri.

Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.

Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.

Taarifa ya Makene ilisema kuwa “leo Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Mhe. Frederick Sumaye akiongozana na viongozi wa chama na madiwani wa CHADEMA, alikuwa na ziara ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na CHADEMA. Katika hali ambayo haijatolewa sababu zozote za msingi, baada ya Mhe. Sumaye pamoja na viongozi wengine kupata taarifa fupi kutoka kwa Meya Boniface Jacob ofisini kwa Meya na walipokuwa wakitoka kuanza ziara, msafara wao umezuiwa na polisi maeneo ya Ofisi za Halmashauri ambapo OCD amemuomba Meya afike kituoni kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala kadhaa kwa muda usiozidi dakika 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *