Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amelezea tukio la bomoa bomoa linaloendelea katika maeneo ya Kimara na kuathiri wakazi wake kuwa ni la uonevu na lenye kubebwa kisiasa.

Boniface Jacob amesema kitendo hicho kimekuwa cha uonevu kwa sababu kesi bado iko mahakamani, lakini serikali imetoa amri nyumba hizo zibomolewe, bila kusubiria hatma ya kesi.

Boniface Jacob pia ameelezea tukio hilo limebebwa na sura ya kisiasa na kusema kuwa kitendo cha wakazi wa maeneo hayo kuwa upande wa vyama vya upinzani ndiyo umewagharimu, na kufanyiwa vitendo vya uonevu wa hali ya juu.

Eneo la Kimara kumefanyika zoezi la kubomoa nyumba na ambalo limeonekana kuathiri kiasi kikubwa cha wakazi wa maeneo hayo, na kuibua malalamiko mengi kwa watanzania ambao hata siyo wakazi wa maeneo haya.

Kwasasa Mahakama imesitisha bomoabomoa katika maeneo hayo baada ya wakazi kufungua kesi dhidi ya serikali kupinga bomoabomoa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *