Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri Kiswahili kitumike kufundishia elimu ya sekondari ili kuwasaidia wanafunzi kujua lugha yao ya Taifa.

Meya Isaya alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi, wakati wa kumbukumbu ya Meya wa kwanza Mwafrika, Kaluta Amri Abeid iliyofanyika nyumbani kwake Magomeni.

Amesema kwamba Taifa limezembea kuitumia lugha ya Taifa na badala yake kutumia Kiingereza jambo ambalo Meya Mwita, anaona ni kupoteza sifa ya Taifa.

Amefafanua kwamba Taifa bado lina changamoto kubwa ya lugha ya Taifa kutokana na kukosekana kwa misingi ya kuwasaidia wanafunzi jambo ambalo linafanya kuwepo kwa ugumu wa kutambua lugha na hivyo kama ingetumika lugha moja ingekuwa ni njia moja wapo ya kulitangaza taifa la Tanzania.

Amesema hao tunaotumia lugha zao, ndio watakuja nchini na kwingine duniani kujifunza kiswahili.

Alisema kwamba wanafunzi wengi wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma lakini hupata nafasi za kuingia sekondari, jambo ambalo huwapa shida kutokana na kujifunza vitu viwili kwa wakati mmoja.

Akizungumzia nafasi ya Meya Shehe Kaluta, Mwita amesema licha ya kwamba hajawahi kumuona, ila kupitia vitabu vyake ambavyo amesoma atahakikisha kwamba anafanya mazuri ili watu waweze kumkumbuka kutokana na yale ambayo atafanya.

Ameongeza kwamba viongozi wote kupitia vitabu ambavyo amesoma, amegundua kwamba yeye na Kaluta ndio mameya wadogo ukilinganisha na wale ambao walipita kwenye nafasi hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *