Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za rambirambi kwa wafiwa  badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Meya huyo amesema kuwa kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5 kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.

Lazaro amesema hayo leo Jijini Ausha wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi.

Amesema fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja kwa moja badala ya kwa RC Gambo.

Amesema wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga  jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.

Naye  Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya hatafika mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *