Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Forums, Maxence Melo mpaka muda huu bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi na hajafikishwa mahakamani mpaka sasa kama sheria inavyotaka.

Melo alifanyiwa mahojiano jana usiku kwa muda mrefu na faili lake lilikuwa linaandaliwa ili lifikishwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Hadi muda huu, mawakili wake hawajapewa hati ya mashtaka hivyo hawajui Melo anashikiliwa kwa makosa gani na atafikishwa mahakamani lini.

Melo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam tangu juzi Jumanne kwa madai ya kugomea agizo la muda mrefu la jeshi hilo.

Polisi wanadai wamekuwa wakiagiza na kuamuru kupewa taarifa za watumiaji wa JamiiForums bila mafanikio.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *