Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ametengua uamuzi wake wa kustaafu soka la kimataifa baada ya kutangaza kurejea kuitumikia timu yake ya Taifa ya Argentina.

Mshambuliaji huyo amerejea kuchezea Argentina baada ya kocha mpya wa timu hiyo Bauza, mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kumtaka arejee kwani umri wake wa kustaafu soka la kimataifa bado ujafika.

Messi alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa fainali ya kombe la Copa Amerika zilizofanyika nchini Marekani ambapo Argentina walifungwa fainali dhidi ya Chile kwa mikwaju ya penati.

Messi: Baada ya kukosa penati dhidi ya Chile kwenye fainali ya kombe la Copa America nchini Marekani.
Messi: Baada ya kukosa penati dhidi ya Chile kwenye fainali ya kombe la Copa America nchini Marekani.

Kocha wa Argentina Bauza amefurahishwa na kitendo cha mshambuliaji huyo kurejea kuitumikia timu hiyo ambapo kocha huyo anatarajia kuita kikosi cheke kwa ajili ya mechi za kufuzu kombe la dunia nchini Urusi.

Agrgentina inatarajia kucheza mechi mbili za kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi dhidi ya Venezuela na Uruguay zitakazofanyika mwezi septemba mwaka huu.

Argentina kwasasa ndiyo timu inayoongoza kwa ubora wa viwango duniani ikifuatiwa na Ubelgiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *