Barcelona imeifunga Celtic 7-0 kwenye mechi ya klabu bingwa barani Ulaya iliyofanyika jana usiku katika uwanja wa Nou Camp.

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi raia wa Argentina amefunga ‘hat-trick’ yake ya sita katika mechi ya kundi C dhidi ya Celtic kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya jana usiku.

Mshambuliaji huyo alianza kwa kufunga bao la mapema mnamo dakika ya tatu ya mchezo huyo nakuifanya Baca kuanza kuongoza mapema.

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili.

Barcelona: Wakishangilia moja ya goli lao kwenye mechi dhidi ya Celtic jana.
Barcelona: Wakishangilia moja ya goli lao kwenye mechi dhidi ya Celtic jana.

Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki na Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.

Katika misimu miwili ambayo wamekuwa pamoja Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez wamefunga mabao 253 na kusaidia ufungaji wa mabao 120.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *