Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameipeleka klabu yake kileleni mwa msiamamo wa ligi kuu nchini Uhispania baada ya kushinda mbili kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Real Madrid.

Kiungo wa Brazil Carlos Henrique Casemiro alifunga goli la kuongoza la Real Madrid kisha Lionel Messi, akasawazosha goli hilo.

Ivan Rakitic akaiongezea Barca, goli la pili katika dakika ya 73 ya mchezo kabla ya mshambuliaji James Rodriguez wa Real Madrid, kuchomoa goli katika dakika ya 86.

Katika dakika ya 90 Lionel Messi, aliifungia timu yake bao la ushindi na hivyo timu yake inarejea kilele mwa ligi wakiwa na alama 75 huku madrid wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 75, wakitofautiana idadi ya magoli na Real wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Madrid walicheza pungufu katika mchezo huu baada ya beki wake kisiki Sergio Ramos, kupewa kadi nyekundu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *