Meneja wa Yamoto Band, Chambuso amefunguka kwa kusesma kuwa kundi hilo bado linafanya kazi pamoja na tetesi zinazoendelea za kuvunjika kwa kundi hilo si za kweli.

Chambuso ameweka wazi kuwa fununu zinazoendelea juu ya kundi hilo la muziki kutoelewana kwa sasa siyo za ukweli.

Chambuso amesema kuwa Yamoto Band kwa sasa wamekua na kwamba wana uamuzi wa kufanya vile wanavyo jisikia na suala la nyumba walizojengewa ni za kwao hata kama hawataendelea kufanya kazi na Said Fella.

Pia amesema kwa sasa mashabiki wasubirie ngoma mpya na video nzuri kutoka kwa Yamoto Band kwa kuwa hamna tatizo lolote na uongozi wao na hakuna tatizo lolote baina yao.

Yamoto Band ni kundi la muziki lililojizolea sifa hapa nchini kutokana na ngoma zao kubamba mashabiki  mpaka kupelekea  kushiriki msimu wa Coke Studio nchini Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *