Mtalaka wa staa wa zamani wa kundi la Spice Girls, Mel B, amekanusha vikali madai ya kumshambulia kimwili na kihisia Mel B miaka minne iliyopita.

Mawakili wa Stephen Belafonte wametoa taarifa ya utetezi baada ya staa huyo wa zamani wa Spice Girls kupewa haki ya muda ya kutowasiliana na Belafonte.

Mel B alifungua kesi mahakamani na kueleza kuwa amekuwa muathirika wa ‘vipigo mbalimbali’ na mumewe wa zamani alitishia kuharibu kazi yake kwa kutoa video yake ya ngono.

Mawakili wa Belafonte wamedai kuwa madai hayo ‘hayana msingi na uzushi’.

Madai ya Mel B yanaeleza kuwa vurugu zilianza baada ya kumaliza kwenye nafasi ya pili kwenye shindano la Dancing With The Stars la mwaka 2007 nchini Marekani.

Staa huyo mwenye miaka 41 ambaye ana watoto na Belafonte amedai kuwa alikuwa na alama za majeraha shingoni hali iliyopelekea kuweka vipodozi ili kuficha hali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *