Rapa nyota nchini Marekani, Meek Mill amekanusha taarifa kwamba amehusika katika uvamizi wa nyumba ya aliyekuwa mpenzi wake, Nicki Minaj na kumuibia vitu vyenye thamani ya £140,000 (TZS 390m)

Rapa huyo ameamua kuvunja ukimya baada ya watu wengi kudai kwamba tukio la wizi alilofanyiwa Nicki Minaj nyumbani kwake limesababishwa na yeye kutokana na kuachana kwao.

Wizi huyo kwenye nyumba ya Nicki Minaj umetokea wakati akiwa anasherehekea muungano wao wa Young Money kwenye sherehe iliyofanyika nchini Marekani.

Kutokana na tetesi hizo Meek Mill amesema kwamba “Naonekana kama nawaibia watu?, nina $450k kwenye shingo yangu, $80k mkono wangu, bado naonekana kama nawaibia watu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *