Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amepiga  marufuku mechi zote za Yanga na Simba kufanyikia uwanja a Taifa kutokana na uharibifu wa mageti na viti uliojitokeza jana katika mechi hiyo ya watani hao wa jadi.

Pia Nape amezuia mapato ya timu hizo ya mchezo wa jana kutokana na uharibifu huo.

Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi.
Mashabiki wa Simba wakitawanywa kwa mabomu ya machozi.

Amri hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung’oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.

Katika mechi hiyo timu hizo zilitoka sare ya 1-1 baada ya Yanga kutangulia kwa goli la Amisi Tambwe na baadae Shiza Kichuya kusawazisha dakika za lala salama.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *