Mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal itarudiwa tena baada ya refa aliyechezesha mechi hiyo kufungiwa na Fifa.

Refa huyo raia wa Ghana Joseph Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimia mechi kwa njia isiyofaa.

Refa huyo amefungiwa na FIFA baada ya kuwapa penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1 mwezi Novemba mwaka jana kwa kushika mpira lakini kanda ya video baaadaye ilionyeha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly.

Lamptey alifungiwa maisha mwezi Machi lakini jana Jumatano adhabu hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo.

Lamptey pia alisimamia mechi katika mashindano ya Olimpki huko Rio nchini Brazil mwaka uliopita.

Senegal na Afrika Kusini kwa saa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi la la D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.

Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa meche za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *