Klabu ya Bayern Munich leo itakuwa na kibarua kizito watakapoikaribisha Arsenal kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika uwanja wa Allienz Arena nchini Ujerumani.

Hatua hiyo ya 16 bora itaamua nani anafuzu kwenye hatua ya robo fainali ambapo watarudiana tena wiki moja mbele.

Kuelekea mechi hiyo kocha wa Bayern Munich Carlo Anceloti amesema kuwa anamuheshimu sana kocha wa Arsenal pamoja na kikosi chake kutokana na kuwa bora.

Timu hizo zimekutana mara nyingi kwenye hatua ya mtoano ambapo mara nyingi Bayern Munich anaibuka na ushindi kwenye mechi nyingi wanazokutana.

Mechi nyingine ya ligi hiyo inawakutanisha Real Madrid na Napoli kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu usiku wa leo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *