Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema wanatarajia kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa Bunge wa kuwasimamisha kutofanya shughuli za kibunge kwa mikutano mitatu mfululizo.
Mdee na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema), waliadhibiwa kwa makosa ya kudharau kiti cha Spika wakati bunge lilipokuwa likijadili kuhusu ripoti ya kamati.
Mdee alitoa kauli hiyo mjini Dodoma jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.
Mdee amesema kuwa “Mahakama ni chombo pekee kilichoundwa na Katiba ili kusimamia haki, hivyo tunaamini Mahakama itatenda haki,” alisema Juni 5, mwaka huu Mdee na Bulaya walisimamishwa kutohudhuria vikao vyote vya Bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti, Aprili mwaka 2018/19.
Hukumu hiyo baada ya kupitishwa na Bunge kwa azimio la pamoja na Spika Job Ndugai alisema hatua hiyo inalenga kuongeza nidhamu kwa wabunge wote.
Mdee na mwenzake walitenda kosa Juni 2, mwaka huu wakati bunge lilipokuwa likijadili Makadilio ya matumizi na mapato ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2017/2018.