Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  (Chadema) jana jioni alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwake Makongo Juu jijini Dar es Salaam kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi na kupelekwa katika Kituoni cha Polisi Oysterbay.

Katibu wa CHADEMA jijini Dar, Henry Kilewo amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA).

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jana aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumweka ndani Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima James Mdee.

DC Hapi ameagiza Mdee kukamatwa kwa madai kuwa kauli yake aliyoitoa juzi, Jumatatu wakati akiongea na wanahabari ni ya uchochezi na ya kumfedhehesha Rais John Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *