Mbunge wa Kawe jijini Dar es Salaam (Chadema), Halima James Mdee amepinga kauli na msimamo wa Rais Dkt. John Magufuli kuhusu wanafunzi wa kike kurudi shule baada ya kujifungua.

Rais Magufuli aliyoitoa kauli hiyo akiwa ziarani mkoani Pwani kuhusu agizo la wanafunzi wanapopata mimba na kujifungua wasiruhusiwe kurudi shule kusoma.

 Mdee ameupinga msimamo huo huku akimtaka rais afuate sheria na katiba ya nchi inayowaruhusu watoto hao warudi shule baada ya kujifungua.

Mdee amesema kuwa anashangazwa na Waziri wa Afya, Dkt. Ummy Mwalimu ambaye amesema agizo hilo kuwa lisiendelee kuzungumziwa wakati wanaoumia ni watototo wenyewe ama kwa kubakwa na kusababishiwa ujauzito na hivyo ya Ummy inawanyima haki watoto kuendelea na masomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *