Mbunge wa Jimbo la Kawe Jijini Dar es Salaam, Halima Mdee amelishauri Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Kamati Teule ili kuchunguza mkataba wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).

Mhe. Mdee ametoa pendekezo hilo leo bungeni mjini Dodoma wakati akichangia mjadala wa taarifa ya CAG iliyowasilishwa na kamati za bunge za Hesabu za Sekali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) huku akituhumu uongozi uliopita wa Jiji la Dar es Salaam kuhusika katika utata wa mkataba huo.

Pia Mdee amehoji kuhusu sakata la mkataba wa Lugumi huku akiishangaa kamati ya bunge ya hesabu za serikali kuliweka kiporo suala hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *