Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amekamatwa na jeshi polisi na kufanyiwa upekuzi wa mara pili ndani ya nyumba yake iliyopo jijini Dar es Salaam.

Upekuzi huo ni mara ya pili kwa Mchungaji huyo baada ya mara ya kwanza kufanyiwa upekuzi kutokana na tuhuma za kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu kujihusisha na madawa ya kulevya.

Hatu ya kukamtawa kwa mchingaji inakuja baada ya kusambaza taarifa zisizokuwa rasmi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatumia vyeti feki vya elimu kwa jina lake kamili ni Daud Bashite na si Paul Makonda.

Mchungaji huyo alisema kuwa siku ya Jumapili anamuweka hadharani mwalimu aliyemfundisha mkuu wa mkoa huyo ili kuthibitisha uhalali wa jina la Makonda.

Kutokana na taarifa zilizosambaa leo zinasema kuwa mchungaji huyo anashikiliwa na jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *