Kikosi cha usalama cha Nigeria kwenye mji wa Ogun  uliopo kusini magharibi mwa Nigeria, wamemkamata mchungaji mmoja kwa kumfunga mtoto wake kwa mnyororo na kufuli.

Mchungaji huyo anayeishi karibu na kanisa la Atan anatuhumiwa kumfunga mtoto huyo mwenye miaka 9, kwa zaidi ya mwezi mmoja huku akimnyima chakula.

Mchungaji huyo alikuwa analikimbia jeshi la Polisi tangu siku ya Ijumaa ambapo kikosi cha jeshi hilo kilibahatika kumuokoa mtoto huyo baada ya kudokezwa na wasamaria wema juu ya tukio hilo.

Askari: Akionekana akimtoa mtoto ndani aliyefungwa na mchungaji kwa minyororo na kufuli nchini Nigeria.
Askari: Akionekana akimtoa mtoto ndani aliyefungwa na mchungaji kwa minyororo na kufuli nchini Nigeria.

Baada ya kukamatwa, mchungaji huyo amekiri kumfunga mtoto huyo kwa mnyororo na kufuli na  kudai kuwa alikuwa akimfunza adabu ya kutokuiba.

Msemaji wa jeshi la polisi, Muyiwa Adejobi amedai kuwa:

‘Mchungaji amedai kuwa mtoto wake amekuwa na desturi ya kuiba vitu mbalimbali humo ndani hivyo alimfunga ili asiweze kukimbia.’

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *